JANA ulichezwa mchezo wa kukata na shoka ndani ya dakika 90 za kibabe kwa timu zilizojipanga kupata ushindi kwenye mchezo wa kirafiki ili kuweza kutamba mtaani.
Ulikuwa ni mchezo wenye uzito wa mchezo uliochezwa Uwanja wa Bora kati ya timu ya Waandishi wa Habari za Michezo dhidi ya Unitalent dakika 90 za moto.
Kazi ilikamilishwa ndani ya dk 45 za mwanzo ubao ulisoma Waandishi wa Habari za Michezo 2-0 Unitalent habari huku kipa namba moja wa Waandishi wa Habari kuokoa kwa panelti.
Ilikuwa bao la kwanza lilifungwa na mshambuliaji ghali Juma Ayo kwa pasi matata ya Isssa Mbuzi ambaye hakukamilisha dk zote 90 zaidi ya 45 alimpisha nyota mmoja matata anayeitwa Mwalami.
Bao la pili lilipachikwa na Mbwana Mshindo lilikuwa ni shuti mwana ukome kwa kuwa alikuwa katikati ya uwanja na katikati ya msitu wa kijiji cha mabeki ila ngoma ilizama nyavuni.