JOSE Mourinho, Kocha Mkuu wa Klabu ya AS Roma ya nchini Italia Jose Mourinho ‘The Special One’ raia wa Ureno kaweka rekodi mpya kwenye ulimwengu wa michezo.
Kocha huyo mbabe wa kauli ameweza kuzinoa timu mbali Ulaya ikiwa ni pamoja na FC Porto, Chelsea, Inter Milan, Real Madrid, Manchester United na Tottenham Hotspurs.
Mourinho ameweka rekodi ya kuwa kocha wa kwanza kufika katika fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA), Europa pamoja na European Conference League baada ya kuitoa Leicester City kwa jumla ya mabao 2-1 na kufanikiwa kutinga fainali ambayo itachezwa Mei 25, 2022 dhidi ya Feyenoord ya nchini Uholanzi.
Pia kocha huyo amefanikiwa kuchukua Kombe la Uefa mara mbili akiwa na vilabu vya FC Porto pamoja na Inter Milan huku akifanikiwa pia kutwaa Kombe la Europa akiwa na Klabu ya Manchester United baada ya kuichapa Ajax Amsterdam na sasa amefanikiwa kutinga fainali ya Europa Conference League.
Sasa kama akifanikiwa kutwaa taji hilo basi ataweka rekodi ya kipekee ya kuwa kocha pekee aliyetwaa mataji matatu ya mashindano yote yaliyoandaliwa na UEFA.