GUARDIOLA HANA UHAKIKA KABISA

KOCHA Mkuu wa Manchester City, Pep Guardiola amesema kuwa hana uhakika kuwa kama kipigo mbele ya Real Madrid kitaleta madhara ya kisaikolojia kwa wachezaji wake wa Manchester City kwenye mbio za kusaka ubingwa.

City walitupwa nje na Real Madrid na baada ya kipyenga cha mwisho wachezaji walianguka uwanjani kwa huzuni baada ya kushuhudia faida ya mabao yao mawili waliyofunga ikiyeyuka kuanzia dk 90 na 91 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Sasa City wamebakiza kupambana kutwaa ubingwa wa Premier kwa mara ya nne ndani ya miaka mitano iliyopita na watakabiliana na Newcastel United kwenye mchezo wa ligi Jumapili.

“Kwetu sisi sijui? Sijui itakuwaje lakini tunahitaji muda sasa tunatakiwa kukamilisha kazi na watu wetu.

“Wachezaji walijitoa kwa kila kitu tulikuwa tumekaribia sana lakini hatukuweza kufikia jambo hilo hivyo tupo imara na tutafanya vizuri mechi zijazo,”