ARTETA YUPO ARSENAL MPAKA 2025

KLABU ya Arsenal imemuongezea dili jipya Kocha Mkuu Mikel Arteta hivyo atakuwa hapo mpaka mwaka 2025 akikinoa kikosi hicho kinachoshiriki Ligi Kuu England.

Pia kocha wa timu ya Wanawake, Jonas Eidevall yeye atakuwa ndani ya timu hiyo mpaka msimu wa 2023/24 ndani ya timu hiyo.

Arteta, alijiunga na timu hiyo mwaka 2019,ameweza kuiongoza timu hiyo kwenye mechi za Ligi Kuu England ikiwa nafasi ya nne na mechi nne zimebaki mkononi kwa sasa na ina pointi 63 baada ya kucheza mechi 34.

Arteta amesema kuwa anafurahi kuwa ndani ya timu hiyo na matumaini yake ni kuweza kufanya vizuri kwa mechi zijazo pamoja na mashindano mengine ambayo watashiriki.

“Malengo yetu ni kuona kwamba tunaweza kuifanya timu inakuwa imara na inapata matokeo kwenye mechi ambazo itakuwa inacheza na inawezekana hasa kwa hapa ambapo tupo tayari,” .