WAKALA MAARUFU DUNIANI ATANGULIA MBELE ZA HAKI

WAKALA maarufu wa wachezaji raia wa Italia Mino Raiola amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda kwa miezi kadhaa.

Wakala huyo aliyekuwa akiwasimamia wachezaji wakubwa duniani kama Paul Pogba na Zlatan Ibrahimovic amefariki akiwa na umri wa miaka 54.

Raiola alilazwa katika hospitali ya Milan mnamo Januari 2022 na kufanyiwa upasuaji lakini aina ya ugonjwa wake haikubainishwa.

Baada ya kufanyiwa upasuaji inasemekana hali yake haikuwa mbaya kiasi kwamba alipewa muda wa mapumziko kwa ajili ya kuimarika.

Taarifa kutoka katika familia ya wakala huyo imeeleza :”Tuna huzuni kutoa taarifa za wakala bora kuwahi kutokea ambaye amefariki dunia.

“Mino alipambania maisha yake mpaka hatua ya mwisho kwa nguvu zake kama ambavyo alikuwa akiwapambania wachezaji wake madili.

“Aligusa maisha ya wengi kutokana na kazi yake na aliandika historia mpya atika soka la kisasa,hakika tutamkubuka daima.

“Tunawashukuru wote kwa sapoti kwa kipindi chote kigumu kama familia, asante,”.