ULE utundu wa kutamba sasa unakaribia lakini kwa jeshi hili la Yanga na Simba, Aprili 30 unadhani nini kitatokea?
Ngoma inatarajiwa kupigwa kwa watani hawa wa jadi ambapo vinara wa ligi ni Yanga wenye pointi 54 na mabao 35 na Simba wao wana pointi 41 na safu ya ushambuliaji imefunga mabao 23.
Hapa tunakuletea jeshi la Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi na Pablo Franco ambaye ni kocha wa Simba:-
Yanga
Diarra
Alianza kikosi cha kwanza kwenye mchezo wake uliopita mele ya Namungo na alitunguliwa bao na mchezaji wa zamani wa Simba Shiza Kichuya.
Kwenye dabi ya mzunguko wa kwanza ya sare ya bila kufungana alikuwa langoni pia huyu kipa wa Yanga.
Diarra Djigui kacheza mechi 16,dk 1,440 kafungwa mabao 6 na ana cleen sheet 10.
Djuma
Hatma yake itaamuliwa leo kama anaweza kuanza ama la kwa kuwa aliumia kwenye mchezo dhidi ya Namungo ni beki wa kupanda na kushuka.
Djuma Shabani yeye katupia mabao 3 asisti 4 kwenye mechi 17 na kayeyusha dk 1,515
Kibwana
Mechi 9 kacheza na kutumia dk 677 ana pasi moja ya bao, huyu stori zake zipo kwenye kichwa cha Bernard Morrison wa Simba namna alivyogandwa mchezo wa mzunguko wa kwanza.
Bangala
Yannick Bangala jitu fulani hivi limekwenda hewani halafu miguu ya kazi akiwa ana asisti 1 kwenye mechi 16 dk 1,515 kasepa nazo.
Mwamnyeto
Mzawa ambaye ni Nahodha Bakari Mwamnyeto kayeyusha dk 1,533 kwenye mechi 17 za ligi.
Aucho
Khalid Aucho mwili wake umejengekeka kimazoezi na amecheza mechi 13 asisti 3 dk 1,239 yeye ni kiungo wa kutibua na kutengeneza.
Sure Boy
Ngumu kuamini kwmba atapenya kikosi cha kwanza lakini Salum Abouakhari ni miongoni mwa viungo ambao wameanza kuwa kwenye ubora.
Mechi aliyowaka zaidi ilikuwa mbele ya Azam FC alipopiga jumla ya pasi 41 na amecheza mechi 6 akitumia dk 454.
Moloko
Jesus Moloko ni mechi 14 kacheza kayeyusha dk 921 katupia mabao 4 na ana pasi 1 ya bao.
Farid
Farid Mussa ni mechi 15 kacheza akisepa na dk 721 kibindoni ana pasi moja.
Feisal
Kutoka kutokuwa fiti sasa karundi ni Feisal Salum amecheza mechi 17 katumia dk 1,415 katupia mabao 5 na pasi 3 za mabao.
Mayele
Fiston Mayele mzee wa kutetema akiwa ametupia mabao 12 kwenye mechi 20 na kayeyusha dk 1,565 ana asisti 3.
Simba
Mabingwa watetezi wa ligi Simba nao sio wanyonge wana watu wa kazi chini ya Pablo Franco ambaye ni kocha mkuu na kete yake huenda itakuwa namna hii:-
Manula
Air Manula anapenda kuitwa hivyo yeye ni Aishi Manula katumia dk 1,440 kwenye mechi 16 alikaa langoni kafungwa mabao 7 kwenye mechi 7 na amekuanya clean sheet 9.
Kapombe
Mwenye jukumu la kupiga mapigo huru na kumwaga maji ni Shomari Kapombe akiwa alionekana kwenye jumla ya mechi 14 akatoa pasi mbili za mabao na ni dk 1,242 kayeyusha.
Mohamed Hussein
Nahodha msaidizi wa Simba katumia dk 1,366 kwenye mechi 17 katupia bao moja na katoa pasi mbili za mabao yeye ni beki wa kupanda na kushuka.
Inonga
Henock Inonga beki wa kazi ngumu ndani ya Simba amecheza mechi 13 na kasepa na dk 1,055.
Wawa
Pascal Wawa beki mwili jumba mwenye uzoefu wa kutosha huku mwili wake ukiwa na michoro kibao amecheza mechi 8 kasepa na dk 632.
Mkude
Huyu ni kiungo mkongwe akiwa na uzoefu wa kutosha anaitwa Jonas Mkude kacheza mechi 12 dk 767 asisti 2 msimu huu.
Sakho
Pape Sakho mzee wa kunyunyiza yeye katumia dk 669 kwenye mechi 13 katupia mabao 2 ana pasi 1.
Kanoute
Jasiri mwenye ukatili kwenye miguu yake ila sura ya upole kaenda hewani kimtindo wanamuita Sadio Kanoute dk 668 mechi 8 bao 1.
Kagere
Meddie Kagere amecheza mechi 19 katumia dk 983 katupia mabao 7 na pasi moja ya bao.
Chama
Hana zali la kuwa mkali mbele ya Yanga lakini ni kiungo bora wa muda wote ndani ya ligi anaitwa Clatous Chama kacheza mechi 8 katupia mabao 3 kasepa na dk 510.
Morrison
Mzee wa kuchetua kacheza mechi 11 katupia bao 1 na ametoa pasi 2 za mabao.