KIUNGO SAKHO HANA PRESHA KUHUSU YANGA

WINGA wa kimataifa wa Senegal anayecheza Simba, Pape Ousmane Sakho, amesema wala hana presha kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga, huku akibainisha kwamba, anauchukulia mchezo huo kama mingine aliyowahi kucheza.

Sakho ambaye amejiunga na Simba mwanzoni mwa msimu huu, amekuwa moja ya wachezaji bora ndani ya kikosi hicho kutokana na kiwango alichokionesha kwenye mechi za michuano ya ndani na ile ya kimataifa.

Akizungumza  kuhusu mchezo huo, Sakho amesema: “Ni mchezo mgumu na mzuri wenye ukubwa wake, lakini hauna presha kubwa sana kwa upande wangu kulingana na mimi kuufananisha na michezo mingine ya kimataifa ambayo tumetoka kuicheza.

“Matokeo ya ushindi ni muhimu kwetu kwa kuwa itaongeza hamasa ya kupambana zaidi michezo ijayo.”

Leo Aprili 30,2022 Sakho anapewa nafasi ya kuweza kuanza kikosi cha kwanza chini ya Kocha Mkuu, Pablo Franco.

Yanga ni vinara wa ligi wakiwa na pointi 54 na Simba wapo nafasi ya pili wakiwa na pointi 41.