MAPILATO HAYA YANGA V SIMBA ACHA KABISA

MCHUJO mkubwa kwa sasa ambao unaendelea kwa sasa ni kwa mapilato watakaokuwa kwenye mchezo wa Yanga v Simba unaotarajiwa kuchezwa Aprili 30, Uwanja wa Mkapa.

Siku 2 zimebaki kwa sasa na hapa tunakuletea wale waamuzi watano ambao waliwahi kuchezesha mechi zilizowahusu Yanga na Simba na huenda jina moja likapenya kwa wale watakaochezesha dabi ijayo na usiombe ukutane nao kwa kuwa kwao kadi nyekundu ama penalti sio jambo kubwa sana.

Kwa waamuzi ambao walichezesha mechi dhidi ya Simba kadi nne nyekundu zilionyeshwa huku kwa zile tano za awali za Yanga hakukuwa na kadi nyekundu iliyoweza kupatikana.

Hapa tunakuletea mapilato wa mechi tano za ligi za watani hawa wa jadi, Yanga v Simba namna walivyoweza kusimamia sheria 17 za mpira namna hii:-

Ahmed Arajiga

Alichezesha mchezo wa Yanga v Geita,Uwanja wa Mkapa

Kwenye mchezo huu alitoa jumla ya kadi 4 za njano na Yanga ilishinda bao 1-0 ilikuwa Oktoba 2

Mdoe

Omary Mdoe alichezesha mchezo wa KMC v Yanga uliochezwa Uwanja wa Majimaji Songea ilikuwa ni Oktoba 19, ubao ulisoma KMC 0-2 Yanga.

Beki wa Yanga, Yannick Bangala alikuwa miongoni mwa waliooneshwa kadi ya njano kwenye mchezo huo.

Sassi

Herry Sassi alicheza mchezo wa Yanga 2-0 Azam FC uliochezwa Uwanja wa Mkapa na ni kiungo Khalid Aucho alionyeshwa kadi ya njano kwenye mchezo huo.

Ilikuwa ni Oktoba 30 wakati Yanga ikisepa na pointi tatu jumlajumla.

Mwandembwa

Emmanuel Mwandembwa alikuwa mwamuzi wa kati kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Yanga 3-1 Ruvu Shooting.

Kwenye mchezo huu Mwandembwa alitoa penalti moja kwa Yanga iliyofungwa na Djuma Shaban ilikuwa ni Novemba 2,2021.

William

Abel William, alikuwa ni mwamuzi wa kati kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Ilulu, ubao ulisoma Namungo 1-1 Yanga.

Katika mchezo huu William alitoa penalti moja kwa Yanga ilifungwa na Said Ntibanzokiza na beki Bangala aliweza kuonyeshwa kadi moja ya njano.

Mwandembwa

Emmanuel Mwandembwa, alikuwa mwamuzi wa kati kwenye mchezo wa kwanza kwa Simba msmu wa 2021/22 uliochezwa Uwanja wa Karume, Mara dhidi ya Biashara.

Ilikuwa ni Septemba 28,2021 ubao ulisoma Biashara United 0-0 Simba, ni penalti moja iliamuriwa na mwamuzi wa kati jukumu likawa kwa John Bocco ambaye alikosa penalti hiyo.

Pia ni kadi 3 za njano Mwandembwa aliweza kuonyesha kwenye mchezo huo.

Akamba

Joseph Akamba huyu alikuwa mwamuzi wa kati kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Jamhuri,Dodoma ambapo ubao ulisoma Dodoma Jiji 0-1 Simba.

Ni kadi mbili za njano aliweza kutoa mwamuzi huyu na alitoa kadi moja nyekundu kwa mchezaji wa Dodoma Jiji ambaye ni Anuary Jabir ilikuwa ni Oktoba Mosi.

William

Abel William alikuwa mwamuzi wa kati kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa na ubao ulisoma Simba 1-0 Polisi Tanzania.

Ilikuwa ni Oktoba 27,2021 na kwenye mchezo huu William aliweza kutoa penalti moja iliyofungwa na Rally Bwalya na kadi moja nyekundu kwa mchezaji wa Polisi Tanzania.

Pia kiungo wa Simba, Hassan Dilunga alionyeshwa kadi moja ya njano.

Ikambi

Raphael Ikambi alikuwa mwamuzi wa kati kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa ilikuwa ni Oktoba 31,2021.

Ubao ulisoma Simba 0-0 Coastal Union na Ikambi aliweza kuonyesha kadi moja nyekundu kwa beki wa Simba, Henock Inonga baada ya kumpiga kichwa mchezaji wa Coastal Union.

Mwichui

Nassoro Mwichui alikuwa mwamuzi wa kati kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa ilikuwa ni Novemba 3,2021.

Baada ya dk 90 ubao ulisoma Simba 1-0 Namungo FC na aliweza kumuonyesha kadi nyekundu ya moja kwa moja Abdulaziz Makame ambaye alimchezea faulo Shomari Kapombe na Jacob Masawe alionyeshwa kadi ya njano.

@Dizo_Click