KLOPP ANAAMINI NI MAPUMZIKO WAKIONGOZA 2-0

JURGEN Klopp,Kocha Mkuu wa Liverpool alikuwa shuhuda wa vijana wake wakiitungua mabao 2-0 Villarreal katika mchezo wa Nusu Fainali ya kwanza ya UEFA Champions League.

Mbele ya mashabiki 51,586 katika Uwanja wa Anfield kipindi cha kwanza mambo yalikuwa ni magumu kwa timu zote mbili kwa kuwa halikupatikana bao.

Ni Pervis Estupinan Tenorio alijifunga dk 53 kisha dk mbili mbele Sadio Mane alipachika bao la pili ilikuwa dk ya 55.

Vijana wa Unai Emery Villarreal walipambana kwa hali na mali kupenya katika kusaka ushindi ila mambo yalikuwa tofauti.

Nyota wa Liverpool Thiago Alcantra amechaguliwa kuwa mchezaji wa mchezo huo.

Licha ya ushindi huo Klopp amesema kuwa wana kazi kubwa ya kufanya ili kuweza kufika katika hatua ya fainali ya UEFA Champions League.

“Mabao 2-0 dhidi yao sio jambo kubwa kwa kuwa kwa sasa unaweza kusema ni mapumziko na tunajua kwamba tutakwenda kwao ikiwa watatufunga mabao 2-0 kisha wakaongeza wana nafasi ya kwenda fainali, “