SIMBA:BILA VAR,TUNGEKUWA NUSU FAINALI AFRIKA

PABLO Franco, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa isingekuwa ni matumizi ya teknolojia ya Video Assitance Referee, (VAR) Simba ingekuwa imetinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho.

Aprili 24, wawakilishi wa Tanzania kwenye mashindano ya kimataifa walitolewa kwenye hatua ya robo fainali kwa changamoto za mikwaju ya penalti mbele ya Orlando Pirates ambao walishinda penalti 4-3 ambazo walifunga Simba.

Ilibidi mshindi atafutwe kwa penalti kwa sababu walikuwa wamefungana jumla ya bao 1-1, Simba ilishinda Uwanja wa Mkapa na Orlando nao walishindwa kwao Afrika Kusini bao 1.

Kwenye mchezo huo uliochezwa Afrika ya Kusini kulikuwa na matumizi ya VAR kama ilivyokuwa ule wa Dar ambao uliamua penalti kwa Simba lakini Afrika Kusini, kadi ya pili ya njano ya Chris Mugalu iliamuliwa kwa marejeo ya VAR na kusababisha aonyeshwe kadi nyekundu.

 Pablo amesema kuwa VAR imekuja ikiwa kwenye matumizi ambayo hayaleti matokeo mazuri kwa timu na hata matumizi yake bado hayajatoa matokeo.

“Ninaona kwamba tulikuwa tuna nafasi nzuri ya kuweza kufanya vizuri na kusonga mbele ila bahati mbaya kumekuwa na matumizi ya VAR hii imekuja na kuanza kutumika lakini kuna wakati imetumika vibaya, kama isingekuwa VAR ninadhani kwamba tungekuwa nusu fainali.

“Mashabiki wamekuwa wakipenda kufanya kazi na sisi na wamekuwa wakiipenda timu yao katika hili ninaweza kusema kwamba asante kwa kweli kazi hii ilikuwa kubwa na kwa mapenzi makubwa.

“Nimejifunza kwamba kila mmoja amekuwa anapenda kuona tunafanya vizuri na hata tulipopoteza kila mmoja amekuwa akiumia.Mpira sio namna ambavyo mnapata matokeo lakini ni namna ambavyo mnafanya na kusonga mbele.

“Tulikuwa na nafasi kubwa ya kupata matokeo mazuri ila bahati mbaya hatujawa na matokeo.Tulicheza vizuri na tulifanya vizuri ila hatujashinda mchezo wetu ambao ulikuwa ni mzuri na tulijitahidi kufanya vizuri,” amesema Pablo.