KUELEKEA kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi ambao unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa Aprili 30 2022 kazi iwe ni moja tu mpira kuchezwa kwa ustaarabu huku kanuni zikifuatwa.
Imekuwa kawaida kwa wengi kuhudhuria mchezo huu huku miongoni mwao wakiwa na matokeo ambayo wanayajua kwenye vichwa vyao na wakiamini kwamba itakuwa ni vile ambavyo wanafikiiria.
Kama itakuwa hivyo hii ni mbaya kwa sababu matokeo hayapatikani kabla ya mchezo kuchezwa ni mpaka pale mchezo utakapokamilika.
Tunaona kwamba kwa sasa kila timu inafikiria namna itakavyopata nafasi ya kuweza kuibuka na ushindi na kupata furaha baada ya dk 90.
Ngoma itakuwa nzito kwa kuwa hakuna ambaye atakubali kufungwa kirahisi hivyo lazima ushindani uwe mkubwa na kila mchezaji aweze kujituma kupata ushindi.
Yote kwa yote wakati uliopo sasa ni wakati wa maandalizi ya mwisho kabla ya mchezo huo ambao unashikilia furaha na huzuni ya mashabiki wengi.
Wachezaji kwenu imekuwa ni kawaida kutumia nguvu kubwa kwenye mchezo huu na kusahau kwamba inakuwa kazi kubwa kwa sababu kila mmoja anahitaji kuona ushindi kwa upande wake.
Kwa yale makosa ambayo yalitokea kwenye mechi za nyuma basi zinapaswa kuweza kufanyiwa kazi na matumizi ya nguvu yasipewe nafasi na badala yake iwe ni mbinu za wachezaji kucheza kwa umakini.
@Dizo_Click