RUDIGER KUIBUKIA REAL MADRID

KOCHA wa Chelsea, Antonio Conte amethibitisha kuwa beki wa kikosi cha timu hiyo, Antonio Rudiger ataondoka kikosini hapo ifikapo mwisho wa msimu huu.

Klabu ya Real Madrid inapewa chapuo la kuinasa saini ya nyota huyo ambaye ana uwezo mkubwa kwenye suala a kutimiza majukumu yake awapo uwanjani.

Nyota huyo anatajwa kuondoka bure kwa kuwa dili lake litakuwa limeisha hivyo anakwenda kupata changamoto mpya kwenye timu nyingine ambayo atahamia.

Inaelezwa kuwa beki huyo yupo kwenye mazungumzo ya mwisho na Real Madrid na mpaka sasa wamefikia hatua nzuri kwa ajili ya kuinasa saini yake.

Ni mkwaja wa pauni 10.1 milioni ameombwa kulipwa kama mshahara wake kwenye timu hiyo ambayo inatarajiwa kumpa mkataba wa miaka minne.