KIUNGO YANGA AINGIA ANGA ZA AZAM FC

IMEELEZWA kuwa kiungo wa kazi aliyewahi kucheza ndani ya Yanga, Mukoko Tonombe yupo kwenye rada za mabosi Azam FC ili kuweza kuinasa saini yake.

Nyota huyo ni miongoni mwa wachezaji ambao waliweza kufanya vizuri ndani ya Yanga msimu uliopia wakati timu hiyo ilipomaliza ikiwa nafasi ya pili.

Pia alikuwa kwenye kikosi ambacho kiliweza kutinga hatua ya Fainali ya Kombe la Shirikisho na ikapoteza kwa kufungwa bao 1-0 na Simba.

Kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Lake Tanganyika, ni bao la Taddeo Lwanga kupitia pasi ya Luis Miquissone liliweza kuipa ushindi Simba.

Habari zinaleza kuwa mabosi Azam FC wameanza mazungumzo na kiungo huyo ili kuweza kumrejesha kwa mara nyingine Tanzania.

Aliposepa ndani ya Yanga kwa makubaliano maalumu kwa sasa anakipiga ndani ya Klabu ya TP Mazembe ya DR Congo.