TAYARI ile ngwe ya kwanza kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali kwa Simba imeshakamilisha na mpango kazi wa awali umeshakwisha.
Mbele ya mashabiki wao wengi waliojitokeza 60,000, Simba ilifanikiwa kushinda bao 1-0 dhidi ya Kaizer Chiefs kwenye mchezo ambao ulikuwa unahitajika ushindi.
Hapa ni dk 90 za mwanzo nyumbani na kuna dk nyingine za kukamilisha kazi ambayo ilianza kufanyika shughuli ijayo sio ndogo.
Ninaona kwamba kuna habari zinazungumzwa kuhusu ushindi wa Simba kwa sasa hilo halipaswi kupewa nafasi na badala yake ni kuiombea dua Simba ifanye vizuri.
Ushindi wa bao moja nyumbani uwape hali ya kujiamini na kuongeza juhudi ugenini kwa kuwa wale Orlando Pirates sio timu ya kubeza hata kidogo.
Kocha anapaswa kuona namna gani anaweza kwenda na mbinu nzuri ya kujilinda na kushambulia kwa wakati mmoja kwa kuwa haitakuwa kazi nyepesi hasa kwa wapinzani wakiwa nyumbani na wanahitaji ushindi.
Ninaona kwamba bado utulivu umekuwa ni wimbo wa kila siku hasa ukiona kwamba kwenye mchezo uliopita ni mashuti 17 walipiga haya ni mengi lakini hayakuwa na faida kwa Simba.
Hatua ya mtoano sio muda wa pointi tena ni muda wa mabao ili kuweza kuiuka kwenye hatua ya nusu fanali ambayo ni kubwa na inahitajika kuweza kufikiwa na wengi kimataifa.
Yote haya ni kuweza kuona kwamba kwenye hatua ya robo fainali mchezo wa pili na wa mwisho lile tatizo la kutumia nafasi ambazo zinatengenezwa linatatuliwa.
Kama mwendo utakuwa huu kwenye mechi zijazo basi tutarajie kuona kikomo kwa Simba kuwa hatua ya robo fainali jambo ambalo halitakuwa na afya kwa soka letu.
Mipango makini na utulivu kwa wachezaji ni muhimu kwenye kila mechi bila kujali inawezekana vipi kupenya hatua hii kubwa na kufanya vizuri.
Inawezekana na ipo njia kwa Simba kutinga hatua ya nusu fainali lakini mpaka waweze kufanyia kazi makosa ambayo wameyafanya.
Wachezaji wa Orlando Pirates waliweza kuja na mbinu ya kujiinda mwanzo na mwishon dk 10 hivi walifunguka na waliwapa somo Simba kwamba wao wapo na uwezo wa namna gani.
Kituo kinachofuata ni Afrika Kusini huko wakumbuke kwamba walikutana na Kaizer Chiefs na waliweza kufungwa mabao 4-0 hili liwe somo kwao na wasisahau kwamba Watanzania wanahitaji kuona wakishinda.
Nina amini kwamba kwa sasa watakuwa wanajua ambacho wanapaswa kukifanya kwenye hatua ya robo fainali ambayo huwa inakuja kwa mtindo wa kipekee.
Ushindi upo lakini lazima utafutwe kwa udi na uvumba hawa Orlando Pirates sio watu wazuri lazima watafutiwe uzuri ili wawe wazuri kwenye mchezo wao ujao na wa mwisho kwa Simba katika kutoa maamuzi.