WAKIWA ndani ya Uwanja wa Stamford Bridge mbele ya mashabiki 32,249 Arsenal wamegoma kuchana mkeka na badala yake wameishushia kichapo Chelsea ikiwa nyumbani.
Baada ya dk 90 ubao ulisoma Chelsea 2-4 Arsenal katika mchezo wa Ligi Kuu England uliokuwa ni wa kukata na shoka.
Mabao ya wenyeji Chelsea yalifungwa na Timo Werner dk 17 na Cesar Azpilicueta dk 32 huku yale ya Arsenal yakifungwa na Eddie Nketiah aliyefunga mawili dk ya 13 na 57,Emile Smith-Rowe dk ya 27 na Bukayo Saka dk ya 90+2 kwa mkwaju wa penalti.
Ushindi huo kwa Kocha Mkuu Mikel Arteta ni muhimu kwake kwa kuwa amesepa na pointi tatu muhimu ugenini na kufikisha pointi 57 ikiwa nafasi ya 5 huku Chelsea ikibaki na pointi 62 nafasi ya 3.
Huku mchezaji bora wa mechi hiyo ambaye alikuwa ni shujaa ni Nketiah wa Arsenal.