MANCHESTER CITY YAIWINDA SAINI YA HAALAND

IMEELEZWA kuwa Klabu ya Manchester City inahitaji kuinasa saini ya Erling Haaland ili kuweza kuwa naye ndani ya kikosi msimu ujao.

Hesabu hizo zinakuja baada ya msimu huu kukosa saini ya Harry Kane mwaka uliopita.

Euro 75 milioni zimewekwa mezani ili kumpata nyota huyo wa Borussia Dortmund pia na Real Madrid wanatajwa kuhitaji saini ya nyota huyo.

Lakini hesabu kubwa kabisa kwa Real Madrid ni kupata saini ya Kylian Mbappe wa PSG.