MENEJA wa Mchezaji wa Yanga Bakari Mwamnyeto aitwaye Kassa Mussa amedai Klabu ya Simba inamsumbua sana juu ya uwezekano wa kumsajili mteja wake ambaye ni mchezaji na nahodha wa Klabu ya Yanga Bakari Mwamnyeto.
Mussa amesema kuwa Simba wameweka mezani ofa kubwa mno ya kutaka kumsajili mchezaji huyo na mbali na Simba Mwamnyeto amepata ofa nyingine zaidi ya tatu kutoka mataifa ya Ugiriki na Malta.
“Simba wanasumbua sana nisiseme uongo, wamekuwa wakiibuka na ofa kubwa kubwa, ofa yao ni kubwa hasa ambayo nayo tumeamua kuichukua na kuendelea kuifanyia kazi.
“Ukiacha Simba, Bakari ana ofa nyingi sana, kuna ofa tatu au nne hivi, kuna klabu ya Ugiriki, Malta na nyingine moja bado tunazungumza nazo,” amesema meeneja wa Bakari Nondo Mwamnyeto
Mwamnyeto ni moja ya mabeki amao wamezidi kuwa imara kila leo baada ya kujiunga na Yanga akitokea Coastal Union.
Mshikaji wake Ibrahim Ame alijiunga na Simba na kwa sasa yupo zake Mtibwa Sugar akiwa huko kwa mkopo.