KOCHA ORLANDO PIRATES AGOMEA USHINDI WA SIMBA

KOCHA wa Orlando Pirates, Mandla Ncikazi amesema Simba imewahujumu kwenye mchezo wao wa kimataifa waliocheza jana Uwanja wa Mkapa.

Baada ya dk 90, ubao ulisoma Simba 1-0 Orlando kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali ya kwanza uliokuwa na ushindani mkubwa.

Kocha huyo amesema:”Kama wameshinda basi kwa penalti ambayo naona kwamba sio sawa kwani walileta VAR ili iweze kutumika na ninaona kwamba haijatumika kwenye mchezo wetu hasa kwenye penalti iliyotolewa.

“Ukweli ni kwamba sisi tulipaswa kupata penalti kwenye mchezo huo ila hatukuweza kupata penalti hiyo hivyo ninaona kwamba hatujatendewa haki kwenye mchezo wetu.

“Ipo hivi VAR kwetu haijatumika na hatujafungwa kwa halali mchezo wetu huu basi kwa kuwa mwamuzi ameamua iwe hivyo hakuna namna yote matokeo tunayachukua,”

Penalti ilifungwa na Shomari Kapombe na msaabisha penati alikuwa ni kiungo Bernard Morrison ilikuwa dk ya 66 Uwanja wa Mkapa.

Kibarua walichonacho Simba ni Aprili 24 nchini Afrika Kusini kusaka ushindi ili waweze kutinga hatua ya nusu fainali.