KAGERA SUGAR YAGAWANA POINTI NA KMC,KAITABA

KWENYE mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Kaitaba Aprili 17 milango ilikuwa migumu kwa timu zote mbili.

Baada ya dk 90 ubao wa Uwanja wa Kaitaba ulisoma Kagera Sugar 0-0 KMC.

Matokeo hayo yanaifanya Kagera Sugar kufikisha pointi 26 nafasi ya 5 baada ya kucheza jumla ya mechi 20.

KMC inafikisha pointi 24 nafasi ya 8 katika msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Vinara ni Yanga wenye pointi 51 baada ya kucheza mechi 19 huku mabingwa watetezi Simba wakiwa nafasi ya pili pointi 41.