UWANJA wa Wembley umesoma Chelsea 2-0 C.Palace mbele ya mashabiki 76,238 Chelsea inakata tiketi ya fainali ya Kombe la FA itakutana na Liverpool.
Mabao ya Ruben Loftus dk 65 na Mason Mount dk 76 yametosha kuipa ushindi timu hiyo.
Jumapili ya Pasaka imekuwa furaha kwa Chelsea baada ya ushindi huo katika mchezo wa nusu fainali.
Sasa Chelsea inatarajiwa kumenyana na Liverpool katika mchezo wa fainali unatarajiwa kuchezwa Mei 14,Uwanja wa Wembley.