WATANZANIA wameombwa kujitokeza kwa wingi kwenye Ligi ya Soka ya Ufukweni ambayo inaendelea katika Fukwe za Coco Beach Dar kwa kuwa ni burudani tosha.
Bonifase Pawasa ambaye ni Mratibu wa Mashindano na Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania ya Soka la Ufukweni amesema kuwa hamasa imekuwa kubwa kwa wanaofuatilia huku akiwaomba wale walioshindwa kufika wajitokeze.
“Hamasa ni kubwa na mashindano yanaendelea mpaka Jumatatu ya Pasaka tutakuwepo hapa kwenye fukwe kuweza kushuhudia ushindani kwa timu ambazo zinashiriki.
“Hakuna sehemu ya kuweza kupata muda mzuri na kuweza kupata burudani zaidi ya hapa Coco Beach kwa sasa na kama kuna mkazi yupo Dar hajafika Coco Beach huyo bado hajafika Dar.
“Utulivu ni mkubwa na mabadiliko yaliyopo ni makubwa Coco Beach ya sasa sio kama ile ya zamani na itawapa muda mzuri wakazi watakaokuja kuona namna ligi inavyokwenda,” amesema Pawasa.
Matokeo ya kundi A kwenye mechi ambazo zilichezwa Aprili 15,2022 Uwanja wa Fukwe za Coco Beach ilikuwa ni Vingunguti Kwanza 5-2 Savannah Boys, PCM Buza 11-1 DSM Footbal Center na Ilala FC 3-2 Friends Of Mkwajuni.
Kundi B wao walikiwasha jana ambapo matokeo ilikuwa ni Msasani Mabingwa 7-2 Mshikamano City,Friends Rangers 7-1 Sayari na Kijitonyama 6-9 Kisa FC,