KOCHA MTUNISIA AITABIRIA MAKUBWA SIMBA KIMATAIFA

ADEL Zraine, raia wa Tunissia ambaye ni mtaalamu wa masuala ya viungo amesema kuwa Klabu ya Simba itafika mbali kwenye mechi za kimataifa.

Kwa sasa Simba ipo hatua ya robo fainali ambapo inatarajiwa kutupa kete yake ya kwanza Aprili 17 dhidi ya Orlando Pirates, Uwanja wa Mkapa.

 Zraine ambaye aliwahi kuwa kocha ndani ya Simba amesema kuwa anaona kabisa timu hiyo ikifanya makubwa kimataifa.

“Ikiwa utakuwa unakumbuka niliwahi kusema mapema kwama Simba itakwenda hatua ya robo fainali na imekuwa hivyo kutokana na kuwa wazuri kwenye mechi za nyumbani.

“Hatua ambayo wapo ni nzuri na nina amini kwamba kuna jambo kubwa litatokea juu yao hasa kwenye hatua hii ambayo wapo na watafanya vizuri na kwenda mbali kwenye mashindano haya wanapaswa pongezi na kujituma zaidi,” amesema Zraine.

Pablo Franco, Kocha Mkuu wa Simba leo ana kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Orlando bila ya uwepo wa Joash Onyang pamoja na Sadio Kanoute.