MICHUANO ya Tanzania Football Federation Beach Soccer Super League, imeendelea kulindima jioni ya leo katika eneo la Coco Beach, Masaki jijini Dar es Salaam, ambapo Jumla ya timu Sita zimeshuka Dimbani.
Mchezo wa kwanza ambao ulianza saa 9:00, ulikuwa ni Dhidi ya Savana Boys ya Yombo Makangarawe na PCM Sports Club ya Buza, mchezo ambao umemalizika kwa Savana Boys kuibuka na ushindi wa mabao 7-6.
Mchezo wa pili ulikuwa ni dhidi ya Vingunguti Kwanza FC na Ilala FC, ambao umemalizika kwa Ilala FC kushinda kwa bao 2-1, kisha zikaingia Uwanjani timu ya Dar FC dhidi ya Friends of Mkwajuni ambazo zimecheza kwa muda wote na mchezo huo wa mwisho kumalizika kwa Friends of Mkwajuni ikiibuka na ishindi wa mabao 7-2.
Ambapo kesho kutakuwa na mechi nne ikianza na mchezo wa kiporo utakaopigwa saa 8:00 mchana kati ya PCM Buza na Ilala FC, kisha zitaanza mechi tatu ambazo ni Sayari FC vs Mburahati FC mchezo utakaonza saa 9:00 Alasili, mchezo wa tatu utakuwa dhidi ya Mshikamano City vs Kijitonyama Sand Heroes kisha Kisa FC vs Friends Rangers ambao utaanza saa 11:00 jioni.