NJOMBE MJI WAANZA NA KICHAPO 8 BORA

WIDDEN Daphet, Kocha wa Njombe Mji amesema kuwa walishindwa kutumia nafasi ambazo walizipata jana katika mchezo wa hatua ya 8 bora.

Huo ulikuwa ni mchezo wa kwanza wa kundi A katika fainali za First League huko Mwanza.

Daphet amesema:”Tulishindwa kupata ushindi kwa kuwa hatukutumia nafasi ambazo tulizipata kwenye mchezo wetu.

“Lakini bado tuna nafasi katika mechi zijazo tutafanyia kazi makosa yetu ambayo tumeyafanya,”.

Alliance ilishinda mabao 2-0 Njombe Mji na Tunduru Korosho iliambulia kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya Rhino Rangers.

Kundi A vinara ni Rhino Rangers huku Alliance ikiwa nafasi ya pili zote zina pointi tatu na Tunduru Korosho ipo nafasi ya tatu huku Njombe Mji nafasi ya nne na hazina pointi.