SIMBA YAGOMA KUWA DARAJA,YAWAITA MASHABIKI KWA MKAPA

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa hautakuwa daraja kwa wapinzani wao,Orlando Pirates ya Afrika Kusini katika mchezo wao wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Simba wanatarajia kuwa wenyeji wa Orlando Jumapili hii kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar na baada ya hapo watarudiana Aprili 24, huko Sauzi

Ahmed Ally, Meneja wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa wamejipanga kufanya makubwa kwenye mchezo huo huku akiwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kuongeza hamasa kwa wachezaji.

“Hii ni mechi kubwa ambayo hakuna Mwanasimba anayetakiwa kubaki nyumbani tunatakiwa tufike kwa wingi ili kuisapoti timu yetu.

“Hatutaki kuwa daraja kwa timu nyingine kutinga hatua ya nusu fainali bali tunataka kuweza kufanikisha jambo mapema na kwa upekee,”.

Ni mashabiki 60,000 ruksa kuweza kuingia Uwanja wa Mkapa kushuhudia mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.