MZEE MAKOROKOCHO AJIBU NI MBILI TU

NYOTA Ibrahimu Ajibu mzee wa makorokocho rekodi zinaonyesha kuwa alijenga ushikaji akiwa ndani ya Simba kwa kuwa aliweza kucheza mechi mbili pekee.

Ajibu hakuwa ni chaguo la kwanza mbele ya Kocha Mkuu, Pablo Franco ambaye alikuwa akiweka wazi kwamba nyota huyo ni moja ya viungo wenye uwezo mkubwa.

Akiwa ndani ya kikosi cha Simba kiungo huyo mzawa aliweza kutumia dk 115 hakuweza kufunga wala kutoa pasi ya bao akiwa na uzi wa Simba

Kwa sasa yupo zake Azam FC ambapo hulo ameshafungua akaunti yake ya mabao akiwa ametupia bao moja ilikuwa mbele ya Tanzania Prisons.

Kwenye mchezo huo Ajibu alianzia benchi na Azam FC ikiwa Uwanja wa Nelson Mandela ilibuka na ushindi wa mabao 4-0 na kuepa na pointi tatu mazima.