YANGA WATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO

YANGA inatinga hatua ya nusu fainali baada ya ushindi wa penalti 7-6 mbele ya Geita Gold.

Dakika 90 zilikamilika kwa timu zote kufungana bao 1-1 katika mchezo wa robo fainali Kombe la Shirikisho.

Katika mchezo wa leo,Kocha Mkuu Nasreddine Nabi ameonyeshwa kadi nyekundu na mwamuzi wa kati baada ya kupuliza kipyenga cha mwisho.

Sasa Yanga itakutana na mshindi wa mchezo kati ya Simba v Pamba SC utakaopangiwa tarehe katika hatua ya nusu fainali.