YANGA V GEITA KUKIWASHA KWA MKAPA

UWANJA wa Mkapa leo Aprili 10 unatarajiwa kuchezwa mchezo wa Kombe la Shirikisho kati ya Yanga dhidi ya Geita Gold.

Huu ni mchezo wa hatua ya robo fainali na mshindi anatinga hatua ya nusu fainali ili kuweza kusaka timu itakayotinga hatua ya fainali.

Bingwa mtetezi ni Simba akiwa naye yupo kwenye hatua ya robo fainali na mchezo wake utakuwa dhidi ya Pamba SC mchezo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Mchezo wa Simba v Pamba SC ambao ulipaswa kuchezwa Aprili 13 umesogezwa mbele na sasa utapigwa tarehe nyingine sababu ya kusogezwa mbele ni kuweza kuipa nafasi Simba kufanya maandalizi kuelekea kwenye mchezo wa hatua ya Robo fainali dhidi ya Orlando Pirates.