MAYANGA V KAGERE KWENYE VITA YAO LEO

LEO ni mwendo wa msako wa rekodi nyingine kwa nyota wawili ambao ni vinara wa utupiaji kwenye timu zao kati ya Vitalisi Mayanga wa Polisi Tanzania na Meddie Kagere wa Simba.

Mayanga ni nyota wa kwanza kusepa na tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Septemba huku Kagere akiwa hajasepa na tuzo kwa msimu huu kati ya 7 ambazo zimeshatolewa.

Ni mabao 6 ambayo anayo Mayanga na pasi tatu za mabao akiwa ameanza kikosi cha kwanza mechi 15 kati ya 18 ambazo zimechezwa na timu hiyo na alikuwa nje kutokana na kutokuwa fiti.

Kwa upande wa Kagere yeye ametupia mabao 7 na pasi moja ya bao kati ya mabao 23 yaliyofungwa na timu ya Simba iliyo nafasi ya pili kwenye msimamo na amecheza mechi 18.