BREAKING:UWANJA WA MKAPA MASHABIKI 60,000 SIMBA V ORLANDO PIRATES

SASA ni rasmi mchezo wa Simba v Orlando Pirates utakaochezwa Uwanja wa Mkapa lile jumba lote la burudani itakuwa ‘full house’ baada ya ruhusa kamili kutolewa.

Taarifa rasmi iliyotolewa na Simba leo Aprili 8 imeeleza namna hii:”Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limekubali ombi letu la mashabiki 60,000 kuingia uwanjani kwenye mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Orlando Pirates.

“Mchezo huo ambao utapigwa Jumapili ya Aprili 17, 2022 saa 1:00 usiku utakuwa wa kwanza kuchezwa Tanzania ukitumia teknolojia ya VAR.

“Tiketi tayari zimenza kuuzwa kupitia mitandao ya simu,”.

Huu unakuwa ni mchezo wa kwanza ndani ya 2022 kwa Simba kuweza kuruhusiwa idadi hiyo ya mashabiki baada ya janga la Corona kutokea duniani.