CHAMA ATWAA TUZO MBELE YA FISTON MAYELE

CLATOUS Chama kiungo mshambuliaji wa kikosi cha Simba amechaguliwa kuwa mchezaji bora kwa mwezi Machi.

Kwa mujibu wa Kikao cha Kamati ya Tuzo ya Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) kilichokutana mwanzo mwa juma hili kimetoa mapendekezo hayo.

Chama ameweza kutimiza majukumu yake vema katika mechi mbili ambazo aliweza kufunga mabao mawili na Simba ikaweza kusepa na pointi sita mazima.

Ameweza kutwaa tuzo hiyo akiwashinda Fiston Mayele wa Yanga na Frank Kahole wa Mtibwa Sugar alioingia nao fainali.

Chama anakuwa ni mchezaji wa 7 kutwaa tuzo hiyo ambao wengine waliotwaa tuzo hiyo ni Saido Ntibanzokiza,(Februari) Fiston Mayele,(Januari) Feisal Salum, (Oktoba) hawa kutoka Yanga.

Relliats Lusajo wa Namungo,(Desemba) Jeremiah Juma wa Prisons,(Novemba) na Vitalis Mayanga wa Polisi Tanzania(Septemba).