SENZO Mbatha, Mtendaji Mkuu Klabu ya Yanga ameweka wazi kuwa Fiston Mayele atafunga mabao mengi msimu huu.
Mayele ni mshambuliaji namba moja ndani ya kikosi hicho akiwa ametupia mabao 10 na pasi tatu za mabao.
Kiongozi huyo amesema kuwa kutokana na kasi ya Mayele pamoja na mechi ambazo zipo mbele atafunga zaidi ya mabao aliyonayo kwa sasa.
“Nadhani Mayele ana nafasi ya kufunga zaidi hasa ukizingatia kwamba kuna mechi nyingi za kucheza zinakuja kwenye ligi.
“Ninafikiria kwamba atafunga mabao mengi zaidi ni mchezaji ambaye anatimiza majukumu yake vizuri akiwa uwanjani kwa kushirikiana na wenzake na hilo ndilo ambalo tunalifanya,”.
Leo Aprili 6, Yanga ina tarajia kusaka pointi tatu mbele ya Azam FC mchezo unaotarajiwa kuchezwa saa 2:15 usiku.