UKIJICHANGANYA UNAPOTEZWA,LEO ZITAPIGWA MECHI KALI

UKIVURUGA hesabu kwa sasa machungu yanakuwa ni yako mazima kwa kuwa hili ni duru la utimilifu wa yale ambayo yalianza kuundwa mzunguko wa kwanza.

Kuna mechi kali mbili leo zinatarajiwa kuchezwa moja ni ile itakayochezwa Uwanja wa Manungu kati ya Mtibwa Sugar v Kagera Sugar na KMC v Namungo,timu zote zipo kwenye msako wa pointi tatu na kwa sasa ukijichanganya unapotezwa jumlajumla.

Timu zote zinahesabu kubwa na tambo zao zipo hivi:-

Mtibwa Sugar

Hawa wanakutana ukiwa ni mchezo wa kisasi kwa Mtibwa Sugar kwa kuwa walipofunga safari kuwafuata pale Uwanja wa Kaitaba walipoteza pointi tatu.

Oktoba 22,2021 ubao ulisoma Kagera Sugar 1-0 Mtibwa Sugar hivyo leo kazi ni moja msako wa pointi tatu Uwanja wa Manungu.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar,Thobias Kifaru amesema kuwa wanatambua umuhimu wa mchezo na wanachohitaji ni pointi tatu.

“Kazi itakuwa ngumu na kubwa hasa ukizingatia kwamba wanakuja Uwanja wa Manungu,kazi itakuwa moja kuonyesha ule mchezo mzuri na burudani kwa mashabiki.

“Hii ni dabi kubwa ambayo inafuatiliwa kwa ukaribu,kwa upande wa maandalizi yapo sawa na wachezaji wapo kambini wakiendelea na maandalizi ya mchezo wetu muhimu,hatujaanza vizuri ”.

Mtibwa Sugar ina pointi 19 baada ya kucheza mechi 18

Ni mabao 12 ambayo yamefungwa na safu ya ushambuliaji wa Mtibwa Sugar huku ule ukuta ukiwa umeruhusu mabao 16.

Ushindi ni mechi 4 na sare ni 7 sawa na zile ambazo imepoteza kwa msimu huu hivyo hesabu kubwa ni kuweza kuongeza rekodi nzuri.

Mayanja

Brian Mayanja huyu ni mtambo wa mabao ndani ya Mtibwa Sugar akiwa ametupia mabao matatu na ni mechi tano aliweza kuanza kikosi cha kwanza

Ndemla

Eneo la kiungo Kocha Mkuu Salum Mayanga anamuamini Said Ndemla ambaye ameanza kikosi cha kwanza mechi 15 na ametupia bao moja pekee.

Kagera Sugar

Kagera Sugar ina pointi 24 mabao ya kufunga ni 15 yale ya kufungwa ni 15 ikiwa imeshinda mechi 6,sare 6 na kupoteza ni mechi 6

Nyota wao Kagera

Eric Mwijage

Amehusika kwenye mabao manne akiwa amefunga mabao matatu na kutoa pasi moja

Kiiza

Huyu ni mkali akianzia benchi ambapo ametoa pasi mbili alipoanzia sub na alifunga bao moja ilikuwa mbele ya Simba.

Kiiza aliliambia Championi Jumamosi kuwa mechi zote ni muhimu kuweza kushinda hivyo watapambana kupata matokeo.

Luhende

David Luhende huyu ni mkali wa mapigo huru alifunga bao moja kwa mtindo huo ilikuwa mbele ya Biashara United ya Mara.

KMC v Namungo

Mbali ya Mtibwa Sugar v Kagera Sugar pia kuna mchezo mwingine utachezwa kati ya KMC v Namungo FC.

Imetoka kuambulia kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Yanga kwenye mchezo wake uliopita wa mzunguko wa pili na sasa inatupa kete nyingine mbele ya Namungo

Baada ya kucheza mechi 18, KMC ipo na pointi 22, imeshinda mechi 5,sare 7 na kichapo ni kwenye mechi 6 ile safu ya ushambuliaji imetupia mabao 20 na imefungwa mabao 21.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa KMC,Christina Mwagala aesema kuwa wachezaji wanajua mchezo huo utakuwa mgumu.

“Duru yetu ya pili tunataka kufanya vizuri kwa michezo ile ya nyumbani na ugenini,timu ipo bora na inaendelea na mapambano,” .

Namungo

Namungo imekusanya pointi 25 ikiwa imeshinda mechi 6,sare 7 na kichapo kwenye mechi 5.

Safu ya ushambuliaji ina mabao 22 na mtupiaji namba moja ni Rellliats Lusajo imefungwa mabao18 safu yao ya ulinzi.

Oktoba 23,2021 walipokutana Uwanja wa Ilulu walitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1,mchezo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Uhuru.

@Dizo_Click.