HATOKI MTU KWA MKAPA IENDE KWA VITENDO

    UNAAMBIWA mtu kwao hilo lipo kwenye mechi za kimataifa hasa kwa soka letu la Afrika ambalo linakwenda kwa namna ambavyo linataka lenyewe.

    Ipo hivyo wewe kubali kata unaona namna ilivyokuwa kwa Simba walishinda kwa mabao 3-1 dhidi ya ASEC Uwanja wa Mkapa walipowafuata ugenini wakachapwa mabao 3-0.

    Tena ni kwamba hapo ASEC walikuwa nje ya Ivory Coast walikwenda nchini Benin lakini wakashinda tena ushindi wa nguvu huku Simba wakibaki wameduwaa hawaamini macho yao.

    RS Berkane hivyohivyo wao walishinda mabao 2-0 nchini Morocco mbele ya Simba na kuwafanya waamini kazi imekwishwa walipokuja Uwanja wa Mkapa wakakutana na picha la kutisha.

    Ushindi wa bao 1-0 ambalo walipata Simba ni hesabu kubwa kwamba nyumbani timu zinashinda lakini zinashindaje hapo ndipo ugumu upo kwa wachezaji kujibu maswali hayo.

    Wimbo mkubwa kwa sasa ni Uwanja wa Mkapa hatoki mtu sasa ni lazima uweze kuwa kwenye vitendo ili Simba waweze kushinda kwani hakuna kazi nyepesi kupata ushindi kimataifa.

    USGN hawana cha kupoteza unadhani nini kitatokea kwa wapinzani hawa ambao wanakuja kutibua mipango ya Simba kutinga hatua ya robo fainali?

    Dakika 90 ni mwisho wa hatoki kwa Mkapa na hapo itajulikana nani ni nani kama ni mbinu za Kocha Mkuu Pablo Franco zitajibu ama zitabuma itafahamika tu.

    Wachezaji wa Simba wana deni kubwa la kusaka ushindi kwenye mchezo huo ambao sio mwepesi hata kidogo licha ya kwamba watakuwa nyumbani.

    Naambiwa kwamba wamewekewa bonsai hakuna kitu kama hicho bonasi haichezi wanaocheza ni wachezaji hata uweke mkwanja mrefu kiasi gani kisha maandalizi yakawa ni hafifu kitakachopatikana ni hafifu.

    Nina amini kwamba wamejifunza kupitia makosa kwa namna ambavyo wamekuwa wakifungwa kwa mabao ya mapigo huru na namna ambavyo bado hawajawa imara kwenye kutumia mapigo huru.

    Uwezo wao wa kupiga pasi ambao hauleti matunda kwa wakati mwingine ni maumivu kwa mashabiki pamoja na Watanzania kiujumla.

    Washambuliaji kazi kubwa sasa ni kuweza kuona wanatumia zile nafasi ambazo wanazipata huku viungo wao jukumu lao ikiwa ni kutengeneza nafasi kwa ajili ya kuwapa wafungaji wafunge.

    Ingawa watakuwa nyumbani inabidi wakumbuke kwamba hata wageni nao watakuwa uwanjani wakizitumia dk 90 zilezile lazima wawe makini.

    Maandalizi mazuri, nidhamu nje na ndani ya uwanja kutumia nafasi ambazo watazipata baso kazi itakuwa imekwishwa na waatambulia furaha.

    Hapo lile neno Uwanja wa Mkapa hatoki mtu litakuwa limekwenda kwa vitendo ikiwa tofauti watu wataambulia maumivu.

    Utapigwa mpira mkubwa kutoka kwa wapinzani kwa kuwa hawana cha kupoteza hivyo Simba kazi ni kubwa kwenye hili.

    @dizo_click

    Previous articleUKIJICHANGANYA UNAPOTEZWA,LEO ZITAPIGWA MECHI KALI
    Next articleNABI AZIPIGIA HESABU POINTI ZA AZAM FC