KIUNGO WA KAZI NGUMU SIMBA AREJEA

SADIO Kanoute kiungo wa kazi chafu kwenye mechi za kimataifa na zile za ligi amerejea mazoezini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya USGN.

Kanoute alikosekana kwenye mchezo dhidi ya ASEC Mimosas uliochezwa nchini Benin na Simba ilipoteza kwa kufungwa mabao 3-0.

Kwenye mechi za makundi, Kanoute amecheza mechi 4 na kayeyusha dk 329 huku akiwa ameonyeshwa kadi mbili za njano kutokana na mikato yake aliyofanya uwanjani.

Anatarajiwa kuwa miongoni mwa wachezaji watakaocheza dhidi ya USGN Aprili 3, Uwanja wa Mkapa.

Kwa mujibu wa Meneja wa Kitengo Cha Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally amesema kuwa kiungo huyo ameanza mazoezi na wachezaji wengine kwa ajili ya mchezo ujao wa kimataifa.

“Kanoute alikosekana kwenye mchezo uliopita dhidi ya ASEC uliocheza nchini Benin lakini kwa sasa yupo tayari na amejiunga na wachezaji wenzake kwenye mazoezi,”

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa usiku saa 4:00 ambapo usafiri utakuwepo mpaka muda wa kuondoka uwanjani.