ASHA MASAKA AANZA CHANGAMOTO MPYA SWEDEN

MSHAMBULIAJI wa Timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake, Twiga Stars, Asha Masaka ambaye alikwea pipa kwa na kuibukia  Sweden Machi 30 tayari ameshatambulishwa kwenye timu yake mpya na kuanza kazi.

Nyota huyo amepata dili la kujiunga na Klabu ya BK Hacken inayoshiriki Ligi Kuu ya Wanawake Sweden kwa makubaliano na Klabu ya Yanga Princes aliyokuwa akiitumikia awali.

Tayari nyota huyo aliagwa na mashabiki pamoja na viongozi wa timu ya Yanga Princes kwenye mchezo maalumu wa kirafiki dhidi ya Ilala Queens uliochezwa Machi 19.

Ameshaanza mazoezi kwenye timu yake mpya akiwa na uzi wenye rangi nyeusi na njano.