NYOTA YANGA PRINCESS SAFARI ULAYA IMEIVA

MCHEZAJI wa Yanga Princess na Timu ya Taifa ya Wanawake, Twiga Stars Asha Masaka leo Machi 30,2022 ameanza safari kuelekea Sweden.

Mshambuliaji huyo anakwenda kuanza changamoto mpya za maisha katika Klabu ya BK Hacken ya nchini Sweden.

Timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya Wanawake nchini Sweden itakuwa na nyota huyo mzawa ambaye alikuwa ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Edna Lema.

Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) limemtakia kila la kheri nyota huyo kwenye maisha yake mapya ya kusaka changamoto kwenye mpira.

Kila la Kheri Masaka katika maisha mapya.