MISRI YALALAMIKA KUONEWA BAADA YA KUFUNGWA NA SENEGAL

TIMU ya Taifa ya Misri yenye nahodha wake Mohamed Salah imefungashiwa virago katika kuwania kufuzu mchezo wa Kombe la Dunia mbele ya Senegal.

Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Me Abdoulaye Wade ulisoma Senegal 1-0 Misri na bao lilikuwa la kujifunga lilifungwa na Hamdin Fathi dk 4.

Misri iliondolewa kwa changamoto za penalti ambapo ni penalti 3 kwa Senegal na 1 Misri ambao walikuwa wanapewa nafasi ya kuweza kusonga mbele.

Katika mchezo huo wakati wa upigaji penalti ni mwendo wa tochi kwa wachezaji wa Misri zilikuwa zinatembezwa jambo linalotajwa lilisababisha Salah kupaisha penalti yake.

Taarifa iliyotolewa na Chama Cha Mpira Misri,(EFA) imeeleza kuwa wamepeleka malalamiko dhidi ya Senegal kuwa walifanyiwa vitendo ambavyo ni vya manyanyaso kwao.

Carlos Quiroz ambaye alikuwa ni Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Misri amebwanga manyanga baada ya kushindwa kufuzu Kombe la Dunia.