REKODI ZA MASTAA WA SIMBA NA YANGA HIZI HAPA

    BADO kidogo kitaumana Uwanja wa Mkapa kwa watani wa jadi kukutana huku kwa sasa wachezaji wa timu zote mbili wakiwa kwenye msako wa kuongeza rekodi.

    Aprili 30, timu hizo zinatarajiwa kukutana na ule mchezo wa mzunguko wa kwanza walitoshana nguvu bila kufungana na kila mmoja akasepa na pointi mojamoja.

    Sasa rekodi za mastaa wa timu zote hadi sasa kwenye ligi ni kali hivyo mashabiki wengi wanaamini timu yao ina nafasi kubwa ya kushinda tofauti na hapo basi huenda hali ya hewa ikachafuka hasa kama mmoja atakubali kichapo kutoka kwa mtani wake wa jadi.

    Yanga ni vinara wa ligi na bado hawajapoteza mchezo msimu huu wakiwa na pointi 48 kibindoni, hapa ni rekodi za ligi za miamba hii miwili:

    DJIGUI DIARRA

    Mechi 14 alikaa langoni dk 1,260 amefungwa mabao 4, hajafungwa mechi 10, alianza kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza walipokutana na Simba.

    DJUMA SHABAN

    Ni mechi 15 dk 1,347 ametoa pasi mbili za mabao na amefunga mabao 2
    JOB Dickosn Job amecheza mechi 15 ana pasi moja ya bao na ni dakika 1,419 kayeyusha.

    MWAMNYETO

    Ni nahodha wa Yanga, kichwani ana bonge moja ya dongo kwa sasa, anaitwa Bakari Mwamnyeto, ni beki wa kati, amecheza mechi 15 dk 1,353 ni mali yake.

    YASSIN

    Yassin Mustapha amecheza mechi 7 dakika 385 pasi moja ya bao.

    BANGALA

    Yanick Bangala kaenda hewani kimtindo na ni beki wa kazi chafu amecheza mechi 15 dk 1,431, ametoa pasi moja.

    KHALID

    Khalid Aucho amecheza mechi 12 ametupia mabao 2 pasi 2 za mabao na ni dk 1,149 ameyeyusha.

    FARID

    Farid Mussa, kiungo huyu ameanza kurejea kwenye ubora akiwa amecheza mechi 14, kasepa na dk 659, ametoa pasi moja ya bao.

    SAIDO

    Said Ntibanzokiza amecheza mechi 11 mabao 6 na pasi 4 za mabao akisepa na dakika 958 huyu ni kiungo wa kazi.

    MAYELE

    Fiston Mayele amecheza mechi 18 mabao 10, pasi tatu za mabao na ni dakika 1,391 kasepa nazo.

    FEISAL

    Eneo la kati linamhusu, ameyeyusha dakika 1,325 na ni mechi 16 amecheza, ametupia mabao 4 pasi 3 za mabao.

    Simba wao wapo nafasi ya pili kwenye msimamo ni mabingwa watetezi wakiwa na pointi zao 37 na jeshi la kazi lipo namna hii:-

    MANULA

    Aishi Manula ni mechi 15 amekaa langoni amefungwa mabao 6 na hajafungwa kwenye mechi 9, kasepa na dk 1,350.

    KAPOMBE

    Beki wa kazi amecheza mechi 12, katumia dk 1,062, katoa pasi 2 za mabao, anaitwa Shomari Kapombe.

    ZIMBWE

    Mohamed Hussein Zimbwe Jr ni mechi 16 kacheza, kayeyusha dk 1,276, katupia bao moja na pasi mbili za mabao. ONYANGO Joash Onyango ni beki wa kati, amecheza mechi 14, katumia dk 1,260 na ametupia bao 1.

    INONGA

    Beki ambaye alifanikiwa kumzuia Fiston Mayele asiteteme mzunguko wa kwanza Henock Inonga, katumia dk 1,055 akiwa amecheza mechi 13.

    MKUDE

    Mkongwe ndani ya kikosi cha Simba akiwa eneo la kati basi utaona uwezo wake akiwa amecheza mechi 10, Jonas Mkude ametoa pasi 2 kwenye dk 731 ambazo kaziyeyusha.

    SAKHO

    Pape Sakho kiungo mnyumbulifu mwenye mabao 2 katika mechi 12 na dk 624 alizotumia akiwa ametoa pasi moja ya bao.

    KANOUTE

    Sadio Kanoute kiungo aliyepanda hewani ni mwendo wa mguso na kuachia akiwa amecheza mechi 7 na kufunga bao moja katika dk 584.

    CHAMA

    Kiungo wa kazi Clatous Chama amecheza mechi 6 katupia mabao 3 katika dk 390.

    KAGERE

    Mshambuliaji namba moja wa Simba ni Meddie Kagere ametupia mabao 6 na kutoa pasi moja ya bao amecheza mechi 17, dk 917.

    KIBU

    Kibu Dennis amecheza mechi 11 kayeyusha dk 713, katupia mabao 3 pasi 2 za mabao

    Previous articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMANNE
    Next articleISHU YA SUMU KWA MMILIKI WA CHELSEA YATAJWA