LEO Machi 29, benki ya NBC ambao ni wadhamini wa Ligi Kuu Bara ya Tanzania wameingia makubaliano na Shirikisho la Mpira Tanzania kwa ajili ya Bima ya Afya na maisha.
Makubaliano hayo ni maalumu ambapo TFF imeweza kuingia na NBC ili kuweza kutoa bima za afya kwa familia ya michezo.
Bima hizo za afya zinatarajiwa kutolewa kwa wachezaji wa ligi zaidi ya 640 pamoja na wataalamu wa benchi la ufundi.
Bima hizi zitawahusu wachezaji pamoja na familia zao na zitawahakikishia kupata matibabu ndani na nje ya nchi.
Jambo hili ni kubwa na linahitaji pongezi kwa kuwa afya ya mchezaji na familia ya michezo ni jambo la msingi kwa kila mmoja. Tunaamini kwamba pale ambapo itahitaji maboresho zaidi yatafanyika na wapo wengine ambao watajitokeza hivyo ni muhimu kuendelea kuwekeza kwenye michezo.
Wallace Karia ambaye ni Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) ameweka wazi kwamba mambo makubwa yanakuja na yatafanyika hivyo inapaswa kuwa hivyo.
Pia napenda kuwakumbusha wachezaji wapato nafasi ya kuweza kucheza wasitumie nguvu ama kuumizana kwa makusudi hili sio sawa kabisa.
Pia isiishie hapa iweze kufika mpaka kule kwa Ligi ya Wanawake Tanzania ambayo nayo ushindani wake unazidi kuwa mkubwa Tukumbukwe kwamba kikubwa ambacho kinawapa wakati mgumu wachezaji ni kuwa nje wakipambana afya zao.