BANDA ASHINDA TUZO YA MCHEZAJI BORA

KIUNGO wa Simba, Peter Banda ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashabiki kwa mwezi Machi.

Banda ameweza kushinda tuzo hiyo akiwazidi kura nyota wawili ambao aliingia nao katika fainali inayodhamiwa na Emirate Aluminium.

Nyota hao ni pamoja na beki wa kazi ngumu na chafu Shomari Kapombe pamoja na kiungo wa kupekecha Pape Sakho.

Kapombe aliweza kuwa chaguo la mashabiki kwa mwezi Februari baada ya kufanya vizuri katika Kombe la Shirikisho aliweza kutoa pasi mbili na kufunga bao moja.

Kwa sasa Simba ipo kwenye maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya USGN unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Aprili 3.