UONGOZI wa Simba umeweka wazi kwamba suala la mchezaji wa ASEC Mimosas Aziz KI kuweza kusajiliwa na timu hiyo litafanyiwa kazi ikiwa kutakuwa na ulazima wa kufanya hivyo.
Imekuwa ikitajwa kwamba mshambuliaji huyo ambaye aliweza kumtungua kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula nje ndani yupo kwenye rada za mabingwa hao watetezi.
Pia habari zilikuwa zinaeleza kwamba nyota huyo ambaye ana mabao matatu kwenye Kombe la Shirikisho yupo kwenye hesabu za kuwindwa na watani wa jadi wa Simba ambao ni Yanga.
Meneja wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema kuwa mchezaji huyo anahitaji kucheza Simba hivyo watalifanyia kazi jambo hilo.
“Hakuna mchezaji mkubwa ambaye hapendi kucheza Simba,KI Aziz anaipenda Simba hivyo kama itakuwa hivyo tutaweka kila kitu wazi,”.
Simba ilipoteza mchezo wake wa Kombe la Shirikisho kwa kufungwa mabao 3-0 dhidi ya ASEC Mimosas na moja ya bao lilifungwa na nyota huyo.