HUU HAPA MTAMBO WA MABAO BONGO

UWEZO wake uliojificha kwenye miguu yake unarekodi ya kubadili upepo hata akianzia benchi huwa anakuwa bora,alifanya hivyo mara mbili mbele ya Geita Gold na Simba na mechi zote hizi aliweza kutoa pasi za mabao.

Ni Tepsi Evance kiungo mshambuliaji wa Azam FC ambaye ni mzawa mwenye pasi nyingi za mwisho ambazo ni 4 na amekuwa kwenye kiwango makini ndani ya timu hiyo.

Kiungo huyo amefunga mabao mawili kwenye ligi na ni aliwafunga Ruvu Shooting bao moja na Prisons pia aliwafunga bao moja.

Kwa mguu wa kulia katupia bao 1 na mguu wa kushoto bao 1 akiwa nje ya 18 katupia bao 1 na akiwa ndani ya 18 katupia bao 1.

Pasi 4 za mabao

Pasi 1 mbele ya Geita Gold ndani ya 18

Pasi 1 mbele ya Simba nje ya 18

Pasi 1 mbele ya Prisons nje ya 18

Pasi 1 mbele ya Dodoma Jiji ndani ya 18

Miguu ya pasi

Mguu wa kulia pasi 2 za mabao

Mguu wa kushoto pasi 2 za mabao

Mitaa ya pasi

Pasi 2 nje ya 18

Pasi 2 ndani ya 18

Alizoanza kikosi cha kwanza

Kagera Sugar

Mbeya City

Ruvu Shooting

Mbeya Kwanza

Tanzania Prisons

Dodoma Jiji

Biashara United

Coastal Union

Polisi Tanzania