ROBERTO Mancini, Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Italia amesema kuwa hajafurahishwa na kutolewa katika hatua hiyo.
Usiku wa kuamikia leo Timu ya Taifa ya Italia ilifungwa bao 1-0 dhidi ya North Macedonia.
Bao pekee la ushindi lilipachikwa kimiani na Aleksandar Trajkovski dk 90+2 Uwanja wa Renzo Barbera.
Sasa North Macedonia itacheza mchezo dhidi ya Ureno ili kuweza kukata tiketi ya kufuzu kushiriki Kombe la Dunia.
Mancini amesema:”Kwa kilichotokea sijapenda na siwezi kuzungumza juu ya mambo ya wakati ujao,”.