TAARIFA ya orodha ya wachezaji wanaoingiza mshahara mrefu kwenye Ligue 1 imetoka, huku mchezaji nyota zaidi kwenye ligi hiyo, Lionel Messi anayekipiga PSG akishika namba mbili kwa kuingiza kitita cha Euro milioni 3.3 (sawa na Sh bilioni 8.5) kwa mwezi.
Takwimu hizo zilizotolewa na gazeti la L’Équipe zinaonesha kuwa sasa mchezaji huyo raia wa Argentina anapokea nusu ya mshahara ambao alikuwa akipokea Barcelona, ambapo kwa mwaka alikuwa akichota kiasi cha Euro milioni 61 tofauti na sasa anapokea Euro milioni 25 pamoja na bonasi ya Euro milioni 15.
Kwenye orodha hiyo namba moja imeshikwa na Neymar aneyakunja kitita cha Euro milioni nne (sawa na Sh bilioni 10) kwa wiki huku Kylian Mbappe akishika namba tatu akichukua Euro milioni 2.2.
Wengine pia waliosalia kwenye 10 Bora ya orodha hiyo wanatoka PSG kama ilivyo tatu bora, ambapo wa nne ni Marquinhos na Marco Verrati wanaochukua Euro milioni 1.2 kila mmoja, anafuata Achraf Hakimi (Euro milioni 1.8), Keylor Navas (Euro milioni moja), Angel Di Maria (Euro 950,000), Gianluigi Donnarumma na Georginio Wijnaldum wanahitimisha kwa kuchota Euro 916,000 kila mmoja