SIMBA WALIJIPA UGUMU KIMATAIFA NAMNA HII KIMATAIFA

LICHA ya Simba kuwa na umiliki mzuri kwa rekodi kuonyeshwa kwamba walikuwa na asilimia 55 huku wapinzani wao ASEC Mimosas wakiwa na asilimia 45 bado haikuwapa pointi tatu mazima.

Kichapo cha mabao 3-0 kiliwapotezea ramani ya kuwa na uhakikwa wa kutinga hatua ya robo fainali kwenye Kombe la Shirikisho kwa kuwa awali walikuwa wanaongoza kundi wakiwa na pointi 7 lakini sasa wapo nafasi ya 3 wakiwa na pointi zao hizohizo.

Cheki namna Simba walivyojipa kazi ngumu ya kuweza kutinga hatua ya robo fainali kimataifa:-

Kadi za njano ziliwatibua

Nyota wa Simba waliweza kuonyeshwa kadi za njano kutokana na kucheza faulo kwa wapinzani wao ASEC Mimosas ambapo miongoni mwao ni Taddeo Lwanga ambaye alionyeshwa kadi ya njano dk ya 47 ikiwa ni dk mbili tangu angie kuchukua nafasi ya Mzamiru Yassin.

Meddie Kagere mshambuliaji wa Simba alionyeshwa kadi ya njano dk ya 55,Pascal Wawa naye pia alianzia benchi na alipoingia kuchukua nafasi ya Henock Inonga alionyeshwa kadi ya njano dk ya 78.

Aishi Manula naye alikuwa kwenye orodha ya walioonyeshwa kadi ya njano ilikuwa dk 35 baada ya kumchezea faulo mchezaji wa ASEC Mimosas katika harakati za kuokoa mpira langoni mwake.

Shujaa wa mchezo kwa Simba

Manula alifanya kosa mwenyewe dk ya 35 kwa kusababisha penalty lakini aliweza kuokoa pigo la Karim Kanote dk 36 pia aliweza kuokoa penalty ya pili dk ya 89 ilisababishwa na Joash Onyango.

Waliopiga mashuti langoni

Kwa kipindi cha kwanza Simba ilikwama kufanya mashambulizi ya hatari ilikuwa shuti moja pekee lilipigwa na kulenga lango na mpigaji alikuwa ni Kagere dk ya 27.

Kipindi cha pili ni Peter Banda alipiga shuti lililolenga lango ilikuwa dk ya 47.

Mzamiru Yassin ni miongoni mwa nyota waliopiga mashuti kuelekea lango la wapinzani ilikuwa dk ya 14, Bernard Morrison ilikuwa dk ya 66,Wawa alipiga dk ya 76 Inonga dk 10 hawa wote walipiga mashuti ambayo hayakulenga lango.

Mapigo huru tatizo bado

Ilikuwa ngumu kwa Simba kuweza kutumia nafasi za kona ambazo walizipata kwenye mchezo huo pamoja na faulo ambapo hakukuwa na hata moja ambayo iliweza kuleta matunda.

Wapigaji ilikuwa ni Shomari Kapombe ambaye alipiga kona dk ya 8,72 na 75, Banda alipiga kona dk 86.

Rally Bwalya alipiga kona dk ya 9,27 na 28 kona zote hizo hazikuwa na faida kwa Simba hivyo ni tatizo inabidi lifanyiwe kazi.

Kituo kinachofuata

Kazi ya mwisho kwa Simba ni Uwanja wa Mkapa dhidi ya USGN ya Niger na kwa namna yoyote watahitaji kupata ushindi ili kuweza kupata nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali Aprili 3,2022 na ili waweze kutinga hatua ya robo fainali wanatakiwa kushinda.