TUCHEL: JAMESN ANAHITAJI MUDA ILI AREJEE KWENYE UBORA

THOMAS Tuchel, Kocha Mkuu wa Chelsea amesema kuwa nyota wake Reece James hapaswi kujiunga na timu ya Taifa ya England kwa kuwa bado hajawa fiti hivyo akiumia tena nani ataziba pengo lake?

Beki huyo wa Chelsea hakuwa sehemu ya kikosi cha Chelsea ambacho kilishinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Middlesbrough Jumamosi katika mchezo wa FA.

Licha ya beki huyo kutumia dk 147, Kocha Mkuu wa England, Gareth Southgate alimchagua beki huyo katika kikosi cha Timu ya Taifa England.

Tuchel ameonesha mashaka juu ya James kujumuishwa katika kikosi cha England kwa kuwa bado hajawa fiti.
“Maoni yangu ni kwamba hapaswi kwenda. Bado yupo katika mazoezi binafsi. Hakuna mashaka anahitaji zaidi ya wiki moja ili aweze kurudi katika ubora wake. Lakini hili sio kazi ya Timu ya Taifa kufanya hivi,”.