MSAFARA wa viongozi wa Simba pamoja na wachezaji leo Machi 22,2022 wamewasili salama Dar wakitokea Benin walipokuwa na kazi ya kusaka ushindi mbele ya ASEC Mimosas.
Simba chini ya Kocha Mkuu, Pablo Franco ilipoteza mchezo huo kwa kufungwa mabao 3-0 na kupoteza pointi tatu muhimu.
Wakiwa ni wawakilishi pekee kwenye Kombe la Shirikisho wanabaki na pointi 7 baada ya kucheza mechi 5 huku vinara wa kundi D wakiwa ni ASEC Mimosas wakiwa na pointi 9.
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema kuwa mchezo wao dhidi ya USGN ya Niger watatumia kupata matokeo.
“Mchezo wetu dhidi ya USGN ni muhimu kwetu kushinda ili kuweza kusonga mbele katika hatua ya robo fainali,”.
Ili Simba iweze kutinga hatua ya robo fainali inatakiwa kushinda mchezo wake wa mwisho dhidi ya USGN ya Niger, Uwanja wa Mkapa.