AKILI ZA SIMBA SASA NI KWENYE LIGI

KATIKA kuhakikisha wanautetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara, Simba wametamba kurejesha makali yao ya Kombe la Shirikisho Afrika katika Ligi Kuu Bara.

Kwenye ligi vinara ni Yanga wakiwa na pointi 48 baada ya kucheza mechi 18 msimu wa 2021/22.

Simba ipo nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 37 na imecheza mechi 17.

 Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema kuwa licha ya wapinzani wao kuongoza katika msimamo wa ligi, lakini bado wana nafasi ya kubeba taji hilo.

“Katika mashindano ya kimataifa tunajua tuna kazi ya kufanya na Wanasimba wasihofu tutafanya vizuri bila mashaka na kwenye ligi tunajua kuna kazi ipo pia.

“Tulichopanga ni kurejesha yale makali tunayoyafanya katika Shirikisho kuyahamishia katika ligi, tunaamini kiwango cha kila mchezaji wetu, hivyo Wanasimba waondoe hofu,”.

Leo kikosi cha Simba kinatarajiwa kuwasili Dar kikitokea Benin ambapo kilikuwa huko kucheza na ASEC Mimosas na kilipoteza kwa kufungwa mabao 3-0”