SAIDO KUIWAHI AZAM FC

SAID Ntibanzokiza kiungo wa Yanga ambaye alikuwa nje kwa muda kutokana na kutibu majeraha yake anatarajiwa kurejea kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Azam FC.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Aprili 6 utakuwa ni wa mzunguko wa pili Uwanja wa Mkapa.

Kiungo huyo aliumia kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Kagera Sugar na alikuwa na jambo la kuaga ukapera nchini Burundi.

Juzi Machi 19,2022 kiungo huyo aliuaga ukapera kwa kufunga pingu za maisha na Samatha Uwera huko Burundi.

Wakati yeye akikamilisha jambo hilo muhimu timu ya Yanga iliweza kushinda mabao 2-0 dhidi ya KMC kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema kuwa wachezaji wake ambao ni majeruhi wakirejea kwenye kikosi watampa nafasi nzuri ya kupanga kikosi cha kwanza.

“Kuwa na wachezaji ambao wanarudi kwenye ubora hilo ni jambo jema kwa kuwa linaongeza nguvu katika kupanga kikosi cha kwanza,”.